loader-logo

Vitu vya msingi kuzingatia kwa kila mmiliki wa Website

Siku hizi, utengenezaji wa website umekuwa rahisi sana, kuna programu nyingi zinazoweza kukusaidia kutengeneza website, mfano wake ni kama Joomla, WordPress, Drupal nk. Kama ilivyo sehemu nyingine, utengenezaji huu wa Website huwa na matokeo chanya endapo kutakuwa na mipango thabiti kabla ya uanzaji wa utengenezaji wake. Hii inamaanisha kuwa, unatakiwa kufahami vitu msingi kwa website kabla haujaanza kutengeneza au kutafuta mtu wa kukutengenezea.

Katika mipangilio hii, kuna vitu vitakuwa vinafanya kazi chini kwa chini (behind the scene) na kuna vile ambavyo vinaonekana/kutumiwa moja kwa moja na wateja. Muunganiko wake, ndiyo huleta matokeo chanya yatakayokupendeza. Hebu tuangalie vitu hivyo;

1. Web hosting inayoaminika na ya uhakika (Reliable Website Hosting)

Web hosting mara nyingi hufananishwa na mwenye nyumba anayekukodisha frame kwa ajili ya biashara, inakuwaje endapo kila siku nyumba yake imefungwa, inavuja au mlango wa kuingilia wateja ni kadogo hivyo kusababisha msururu wa foleni kwa wateja wanaotaka kuingia madukani.

Web hosting company ya uhakika itahakikisha website yako ipo online muda wote na hata ikitokea imeenda offline, basi ni muda mchache na haijirudii rudii, pia watakuwa wanakupa ushauri pale kunapotokea matatizo na kuhakikisha usalama wa website yako. Haijalishi umetengeneza kwa mtindo gani, hakikisha unapa hosting ya uhakika kulingana na mahitaji yako, iwe ndiyo unaanza na ukachukua kifurushi kama cha Mikumi kinachopatikana Duhosting au kwa wale wenye wateja wengi wakaamua kutumia VPS au cloud, hosting lazima iendane na mahitaji yako. Kuna makala tumeandika Ufahamu Juu Ya Website Hosting Na Tofauti Zake inaweza kukusaidia kukupa mwanga pindi unapotaka kuchagua aina ya hosting inayofaa kwa website yako.

2. Content Management System (CMS)

CMS inakusaidia kuchunga website yako kwa urahisi, CMS ipo kwenye kundi la vitu vinavyofanya kazi chini kwa chini kwa sababu ni admin hutumia kwa ajili ya kufanya maboresho kwenye website. Kwa sasa kuna CMS nyingi na hata unaweza kuamua kutengeneza ya kwako mwenyewe kama wewe ni mpenzi wa code, ila kama utaamua kutumia nyingine zinazopatikana, zipo CMS kama WordPress, Joomla nk. CMS zimesababisha utengenezaji wa website kuwa rahisi sana kwa sababu huja na template kabisa zenye muonekano mzuri.

Ingawa CMS zimeleta uchanya mkubwa kwenye anga ya website, ila pia, zimeleta changamoto kubwa ya usalama kwa watengenezaji goigoi ambao hupachika kila kitu wanachokiona, na pia kuna wengine huokota cms majalalani na kutengenezea website ambazo siku za mwisho huwa si salama na wadukuzi huzivamia na kufanya watakalo.

3. Search Engine optimization (SEO)

Kwa dunia ya sasa, kufanya SEO ni kitu cha lazima, hii ni kwa sababu ushindani umekuwa mkubwa sana, leo hii kuna mamia ya website zinazofanya kitu kimoja, na tena ujio wa Internet umeondoa mipaka, unajikuta ushindani hauishii kwenye mipaka ya Tanzania peke yake, bali unashindana na watu kutoka dunia nzima. Hivyo, ni lazima upambane.

Kumbuka, kila mtu anataka kutokea kurasa ya kwanza kwenye matokeo ya utafutaji wa Google, hivyo si kazi rahisi. Mfano mzuri, Dudumizi tumekuwa kurasa ya kwanza kwa miaka zaidi ya mitatu kwa huduma zetu za Website Design, Website Hosting na hata Domain registration hii ni kwa sababu ya kuifanyia kazi SEO.

Siku hizi, SEO imebadilika sana, unatakiwa sana kuzingatia ubora wa taarifa zako unazoweka mtandaoni, kujua keywords zako, na pia kuhakikisha website yako inafunguka hata kwa watembeleaji wa simu (Mobile ready).

4. Mobile friendly

Takwimu zinaonesha kuwa, watembeleaji zaidi ya 50% wanatumia simu za mkononi kutembelea website, hivyo ni lazima uhakikishe kuwa website yako inafunguka vyema kwenye vifaa vy amkononi kama simu, tablet, laptop ndogo nk. Ukiwa na webiste inayoonekana vyema kwenye vifaa vya mkononi pia itakusaidia sana kwenye SEO kwa kupata maksi zaidi, Google hupenda kurasa zinazosomeka vyema na vifaa vya mkononi.

5. Analytic

Huna usemi wanasema, kama hautopima, basi ni ngumu kuja kuboresha. Analytic zinakusaidia kujua muenendo wa website, pia inakupa taarifa juu ya watembeleaji wanakujaje, hutembelea page zipi na huondokea page zipi, hii inakupa nafasi hata ya kujua wapi uweke tangazo gani.

Tunapoangolea analytic, ni tofauti sana na zile zinazoonesha idadi tuu, mara nyingi wateja wetu wamekuwa wanasema nataka counter kwenye website yangu. Ukiwa na counter pekee, haitotosha kukupa taarifa nzuri zaidi. kwenye analytic unaweza kutumia Google Analytic ambayo pia inapatikana bila gharama yoyote ya ziada.


6. Kuunganisha na Mitandao ya kijamii

Siyo lazima uwepo kwenye mitandao yote ya kijamii, bali unatakiwa kuchagua ile unayoweza kuimuda na kuunganisha na website yako, makala utakuwa unazituma kutokea kwenye website kwenda kwenye mitandao jamii, mtu anayetembelea website yako awe na uwezo wa kuona nini kinaendelea kwenye mitandao jamii. Huu muuunganiko utahakikisha wateja wako wanapata taarifa zenye kujitosheleza na kukuongezea maksi zaidi.

Nini kinafuata?

Baada ya kujua vitu vya muhimu kwenye website, sasa utakuwa na shauku ya kuwa na Website yako, unaweza kupata quotation hapa, na kama utataka kuwa na hosting, tembelea Winestle Solutions.

0 Points


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *